Eneo linalofaa kwa kilimo katika Wilaya ya Ilemela ni hekta 11,074 mpaka sasa eneo linalolimwa ni hekta 5,369 sawa na asilimia 48 ya eneo lote. Mazao yanayolimwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ni; Mpunga, Mahindi, Mihogo, Mtama, Maharage, Kunde na mazao ya bustani. Wakulima wengi wanapata kipato chao kutokana na kilimo cha bustani ambacho kinachukua karibu hekta 37. Shughuli za kilimo zinategemea mvua za msimu na kuna misimu miwili ya mvua ambayo ni; Vuli (Oktoba hadi Desemba) na masika (Januari hadi Mei).
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa