UTANGULIZI
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni moja ya idara nyeti katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutokana na ukweli kwamba asilimia 65 ya wakazi wa Manispaa wanajishughulisha na Kilimo, na kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa. Manispaa ina jumla ya hekta 11,074 zinazofaa kwa kilimo lakini mpaka sasa kilimo kinafanyika ndani ya hekta 6,769 tu. Manispaa inayo mabonde yenye jumla ya hekta 1,072 kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga na matunda. Tunazo fursa nyingi za kutekeleza kilimo ikiwemo uwepo wa Ziwa Victoria kwa ajili ya upatikanaji wa maji, wataalam, masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo na uongozi imara ambao wanatoa mchango mkubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kutafuta wafadhili watakaowasaidia wakulima kuzalisha zaidi na kuongeza kipato chao. Zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo katika Manispaa ya Ilemela. Mojawapo ni wakulima kutegemea mvua, bei kubwa za pembejeo na zana za kisasa, uhaba wa masoko, na uvamizi wa visumbufu vya mazao. Ili kutatua changamoto hizi, ni vema Serikali katika ngazi zote ikatilia mkazo katika upatikanaji wa maji mbadala wa mvua kwani hali ya mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kuwa chagamoto kubwa kwa wakulima. Pia wakulima wasaidiwe kupitia vikundi vyao wenyewe, taasisi za kifedha na wafadhili mbalimbali kupata pembejeo na zana za kisasa ili waweze kuzalisha zaidi.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA
JINSI HUDUMA ZINAVYOPATIKANA
Huduma hizi hutolewa ndani ya Manispaa kwa njia zifuatazo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Anuani ya Posta: 735 MWANZA
Simu: + 255 736 200910
Simu:
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa