1.0 UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara 13 na vitengo 6 vinavyojitegemea katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, na ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za Manispaa.
1.1 MUUNDO WA IDARA
Idara ina vitengo Vikuu Vitatu ambavyo ni:
Idara ina jumla ya watumishi 29 kati yao wanaume ni 9 na wanawake ni 20 na viwango vyao vya elimu ni kuanzia ngazi ya Astashahada hadi shahada ya Uzamili kwenye fani za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu ya Jamii.
1.2 SHUGHULI ZA IDARA.
1.2.1 Maendeleo ya Jamii
Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbali mbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
Kueneza elimu ya Uraia mwema.
Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
1.2.2 Ustawi wa Jamii
Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo, Kanuni na viwango vya ubora katika utoaji wa huduma mbalimbali za ustawi wa jamii.
Kufanya tathmini, ufuatiliaji na utaratibu wa huduma za ustawi wa jamii.
Kujenga uwezo wa kitaaluma kwa Maafisa Ustawi wa jamii ili waweze kutoa huduma timilifu kwa wananchi.
Kufanya tafiti zinazohusu huduma za ustawi wa jamii.
Kuwajengea uwezo watumishi wa ustawi wa jamii na Wadau katika utoaji wa huduma.
Kuanzisha na kuendeleza programu za kushawishi, kutetea na kulinda haki za makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu wa viungo na ngozi, wazee na wasiojiweza, familia zenye dhiki na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Kujenga Uhusiano na wadau wa nje na ndani ili kutoa huduma bora za ustawi wa jamii.
Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
1.2.3 Maendeleo ya Vijana
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.