Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala amesisitiza suala la nidhamu ya matumizi ya fedha Tshs. Bilioni 2.2 za ujenzi wa vyumba vya madarasa iliyotolewa na serikali kuu kwa ajili ya maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023
Amesisitiza hilo wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa maandalizi ya ujenzi wa vyumba hivyo katika Manispaa ya Ilemela.
Mhe Masala amesema kuwa lengo kubwa ni wote kutembea kwenye mlengo mmoja ili kuweza kukamilisha ujenzi wa madarasa haya kwa wakati na kuwa fedha hizi zinahitaji nidhamu katika usimamizi, kwani ni fedha za umma na zimetolewa na kiongozi wetu haipaswi kumuangusha.
“Shilingi milioni Ishirini kwa kila darasa, isiposimamiwa vizuri itamtaka mkurugenzi aongeze fedha na ni kitu sitarajii kitokee hivyo nidhamu ya matumizi izingatiwe”, amesisitiza Mhe Masala.
Pamoja na hayo ameagiza wakuu wa shule wote kuwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa ujenzi , sambamba na hilo ameelekeza kushirikisha wananchi kuanzia uchimbaji wa msingi ili waweze kumiliki miradi hiyo, kufanya ufuatiliaji wa bei elekezi ya vifaa mbalimbali huku akisisitiza kuzingatia suala mgawanyo wa kazi kwa kushirikisha kamati zote .
Aidha amewataka wenyeviti wa mitaa yote kusemea mapokezi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo inaendele kwa wananchi ili waweze kupata uelewa wa fedha zote zinazotolewa na serikali ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Katika nyakati tofauti madiwani wa kata za Bugogwa, Kayenze na Shibula wamemshukuru Mhe . Rais kwa fedha hizi za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani vinaenda kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari.
Akihitimisha Mhe Masala ametoa maelekezo kwa wakuu wa shule kuhakikisha kuwa kila mmoja anatekeleza jukumu lake kwa kuhakikisha kuwa zoezi la ujenzi wa vyumba hivi 110 vya madarasa linakamilika kufikia tarehe 20 mwezi wa kumi na mbilli. , “lazima kuwekeza kwenye elimu kwani ndio kila kitu”, amesema Mhe Masala.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.