• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GESI NISHATI MBADALA RAFIKI WA MAZINGIRA: MHE MABULA

Posted on: September 16th, 2023

"Malengo ya serikali ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ni kwamba kufikia mwaka 2032 wananchi wote wawe wameondokana na nishati zinazodhuru na kupata nishati safi kwa afya zao."


Kauli hiyo imetolewa na Mhe.Dkt.Angeline Mabula(Mb) wa Ilemela alipokuwa akizungumza na kina mama wajasiriamali wa Ilemela katika hafla ya kuwakabidhi gesi kina mama hao.

Mhe.Mabula amesema kuwa ni ajenda ya serikali ya awamu ya sita kumpunguzia mama mahangaiko ya muda mrefu na kumpatia nishati mbadala ya gesi ili kukamilisha kazi zake za upishi haraka na kupata muda wa kufanya shughuli za kujiingizia kipato zaidi kiuchumi.


" Naamini wote tunakubaliana kwamba gesi ni nishati mbadala rafiki wa mazingira, naomba tuwe makini katika matumizi yake ili tusilete athari mbaya katika mazingira yetu."


Sambamba na hayo Mhe.Dkt Mabula ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali za afya, elimu n.k.


Tunawashukuru REA kutoka wizara ya nishati kwa kuunga mkono juhudi za Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya utunzaji wa mazingira nchini kwa kutoa mitungi hii ya gesi." Amesema Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala aliekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.


" Tutaendeleakuunga juhudi za Rais wetu kwani hajatuangusha.Anafanya kazi nzuri inayoonekana ."


Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe.Renatus Mulunga amewaasa wana Ilemela kuendelea kuyaishi mazuri yote yanayofanywa na viongozi wetu kwa kuwa tunaona maendeleo yanavyokuja kwa kasi ndani ya Manispaa ya Ilemela.


Aidha elimu ya juu ya utunzaji wa mazingira imetolewa kutoka kwa mtaalam wa wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ndugu William.

" Ni muhimu kutunza mazingira kwani ndio sehemu tunayoishi.Faida za miti ni nyingi kwetu ikiwa ni pamoja na kupata matunda, vivuli na hewa safi ya oksijeni ambayo ni hewa muhimu kwa binadamu." Amesema William


Anna Masalu ni mama lishe kutoka kata ya Nyamhongolo yeye anamshukuru Mhe.Mabula kwa kutoa gesi hizo.


" Namshukuru Mama Mabula kwa hii zawadi itanisaidia sana katika shughuli zangu za mapishi, yaani sasa hivi mteja akija kila kitu fasta tu."


Jumla ya mitungi 400 ya gesi imetolewa na wizara ya nishati kupitia REA katika kuunga mkono jitihada za mbunge wa Ilemela Mhe.Mabula na kukabidhiwa kwa  kina mama wajasiriamali wa Ilemela.





Announcements

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA 2023- MANISPAA YA ILEMELA November 23, 2023
  • TANGAZO LA MAPOKEZI YA FEDHA KIPINDI CHA KUISHIA MWEZI OKTOBA 2023 November 08, 2023
  • TANGAZO LA BODI YA MFUKO WA ELIMU July 20, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA MANISPAA YA ILEMELA July 13, 2023
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • ILEMELA YAPOKEA MADAWATI 170 NA MITI 1700 KUTOKA DESK & CHAIR FOUNDATION

    December 06, 2023
  • " TUSIONE AIBU KUZUNGUMZA MASUALA YA UKIMWI NGAZI ZA FAMILIA."

    December 01, 2023
  • ALAT MWANZA YAIPONGEZA ILEMELA UJENZI WA BARABARA KWA MAPATO YA NDANI

    November 28, 2023
  • "TUCHUKUE TAHADHARI KIPINDUPINDU KINAUA" - DKT. MARWA

    November 23, 2023
  • Tazama zaidi

Video

TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA EAST BUSWELU
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.