• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MFUMO WA E-BOARD ULIVYOBORESHA UENDESHAJI WA VIKAO ILEMELA

Posted on: May 2nd, 2024

Mwaka 2022 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilianza kutumia mfumo wa E-Board lengo ikiwa ni kurahisisha uendeshaji wa vikao na kupunguza gharama za maandalizi ya vikao hivyo.


Mfumo wa E- Board ambao umesanifiwa na kutengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) hutumika kuwezesha uratibu wa shughuli za uandaaji wa vikao mbalimbali vya bodi na menejimenti katika Halmashauri na Taasisi za Umma .


Kuanza kutumika kwa mfumo huu wa E-Board katika Manispaa ya Ilemela kumesaidia kuokoa matumizi ya fedha nyingi zilizokuwa zinatengwa kwa ajili ya manunuzi ya shajara, wino na vifaa vingine kwa ajili ya maandalizi ya vikao ikiwemo kudurufu taarifa mbalimbali kwani kwa sasa taarifa hizo zinapakiwa kwenye mfumo na kisha madiwani na wataalam  wamekuwa wakipakua kwa ajili ya kuzifanyia kazi, amefafanua Bi Ummy Wayayu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela.


“Kwa mwaka tulikuwa tunatumia takribani shilingi milioni 200 hadi 300 kuandaa vikao, lakini kwa sasa gharama hizo hatuna tena kwani tunatumia  mfumo huu wa e-Board, ambao umesaidia kupeleka fedha hizo katika mambo mengine ya muhimu ya halmashauri,” alisema Bi.Ummy.


Mkurugenzi Ummy ameongeza kusema kuwa mfumo wa e-Board umeweza kuwasaidia madiwani kupokea taarifa ya kikao hata  wanapokuwa nje ya halmashauri hiyo kupitia  vishkwambi ambavyo wamewezeshwa kwa ajili ya matumizi ya mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuweza kujua agenda za vikao na kufuatilia yatokanayo ya vikao na hivyo umeweza kuokoa muda wa kuendesha vikao vya halmashauri.


Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela,  Mheshimiwa Renatus Mulunga, amesema kuwa mfumo wa e-Board umewasaidia madiwani kuendesha vikao vyao kwa ufanisi ili kuboresha huduma za wananchi wa Ilemela. Na hivyo kutoa rai kwa halmashauri nyingine ambazo bado hazijaanza kutumia mfumo wa e-Board, kufanya ziara halmashauri ya Manispaa ya ilemela ili kuweza kujifunza au kuwasiliana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ili zipate uelewa kuhusu mfumo huo.


Sara Lisso ni Diwani wa viti maalum yeye amepongeza matumizi ya mfumo huu kwani ni rahisi kutumia na popote ulipo unaweza kusoma kikao husika , pamoja na hilo kupitia mfumo wa E-Board umewawezesha madiwani kujihudhurisha kwenye kikao au kuomba udhuru wa kikao popote pale anapokwepo.


Kupitia mfumo huu wa E-board umesaidia kuokoa muda wa kusambaza makabrasha  kwani hapo awali ilibidi kuhakikisha makabrasha ya vikao yanasambazwa kwa madiwani  katika kata zote 19 za Halmashauri. hayo yamebainishwa na Mwandishi wa Vikao Ndugu Shilinde Malyagili.


Tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa E-Board takribani vikao 50 vimeendeshwa  vikao hivyo vimejumuisha vya menejimenti , vya kamati za kudumu na vikao vya baraza la madiwani.


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.