Mkandarasi Nyanza Road Works Ltd ametakiwa kuhakikisha anatekeleza mradi kwa wakati na kwa ubora wenye kuzingatia thamani ya fedha.
Rai hiyo imetolewa na Adv. Mariam Msengi (DAS), akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilemela wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Barabara za Manispaa ya Ilemela kwa mkandarasi.
“ Nategemea kuwa mradi huu utatekelezwa kwa viwango vya juu vinavyokubalika,tukumbuke kwamba serikali imetoa fedha hizi kwa ajili ya kuleta nafuu kwa wananchi wake fedha hizi ni za wananchi hivyo ni wajibu wetu kuzitendea haki kwa kuhakikisha zinaleta matokeo chanya.” Amesema Bi. Msengi
Sambamba na rai hiyo, Adv Mariam amemtaka mkandarasi kuhakikisha anashirikiana na wananchi ambapo mradi unapita ili kuepusha migogoro ambayo itapelekea kuchelewesha utekelezaji wa mradi, huku akiwataka wenyeviti wa mitaa katika kata za Buswelu, Nyamhongolo na Nyakato kutoa ushirikiano kwa mkandarasi na kushiriki kikamilifu ili waweze kuumiliki mradi huu.
Katika nyakati tofauti waheshimiwa madiwani wameishukuru na kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara kwani ni mradi ambao umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na kwa hamu na wananchi wa kata ambazo mradi huu utapita huku wakiahidi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi, sambamba na hilo wamemtaka mkandarasi kuhakikisha anawashirikisha viongozi wa kata.
“ Natoa pongezi kwa uongozi mzima wa Ilemela kwa hatua ya mradi huu ilipofika, ni ahadi ya muda mrefu tuliyoitoa kwa wananchi wa maeneo ya Buswelu juu ya ujenzi wa barabara hizi ni matumaini yangu kuwa kukamilika kwake kutaleta chachu ya maendeleo na kufungua shughuli nyingi za kiuchumi kwa wananchi wa Buswelu na maeneo mengine ya jirani.” Amesema Mhe. Sarah Nghw’ani diwani wa kata ya Buswelu.
Nae diwani wa kata ya Nyamhongolo Mhe. Andrea Nginila amemsihi mkandarasi wa mradi huo kampuni ya Nyanza Roads Works Limited kutoa ajira kwa vijana maeneo mradi unapotekelezwa na kutoa wito kwa wakala wa usafirishaji wa ardhini (LATRA) waongeze ruti za magari kufika kwenye vituo vilivyopangwa sasa na waongeze vituo katika barabara hizo ili kurahisisha maeneo mengi kufikika kwa manufaa ya wananchi wote.
“ Hatuna mashaka na kampuni ya Nyanza Roads Works Limited ni kampuni ya muda mrefu na tumeona kazi zake nyingi nzuri,naomba msituangushe kiwango hicho tunachokifahamu kiendelee katika utekelezaji wa miradi hii ili mzidi kuacha alama na kuturahisishia kuwakumbuka kwa kazi zingine zitakazoendelea kujitokeza.” Amesema Mhe.Winfrida Diwani viti maalum Buswelu.
Mhandisi Juma Marwa (QS) –Meneja mradi kutoka kampuni ya Nyanza Roads Works Limited amesema wamepokea kwa uzito mkubwa maoni yote yaliyotolewa na wadau wa maendeleo katika hafla hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi.
Pamoja na michango hiyo kutoka kwa madiwani wa Ilemela, hafla hii ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka chama cha maafisa usafirishaji, wenyeviti wa mitaa ambpo walipongeza kwa hatua hiyo na kuomba sehemu za maegesho ziwepo katika maeneo ya vituo vya daladala sambamba na uwekaji wa mitaro pamoja na uwekaji wa maeneo ya kujikinga jua/mvua katika vituo vya daladala.
Akihitimisha hafla hiyo mstahiki meya wa manispaa hiyo Mhe.Renatus Mulunga ametoa shukrani nyingi kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ,baraza la madiwani na uongozi mzima wa Manispaa ya Ilemela kwa kufika hatua hiyo ya kuanza ujenzi wa barabara hizo.
“ Ni hatua kubwa naomba tuimarishe ushirikiano mzuri kwa wananchi wa maeneo yote mradi unapotekelezwa ,wao ndio wamiliki
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.