Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia chanzo chake cha mapato ya ndani imeendelea na uboreshaji wa huduma za jamii ikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika sekta ya Afya kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma hiyo ya msingi kwa wakazi wa Ilemela na maeneo ya jirani.
Kituo cha Afya cha Buzuruga ni moja ya kituo cha Afya katika Manispaa ya Ilemela kinachonufaika na mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo kimetengewa kiasi cha Tsh Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi hadi kukamilika.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la wateja wanaofika katika kituo hiki kutokana na maboresho yaliyofanyika mwaka 2020 ya huduma ya upasuaji ambapo kituo kilianza kupokea idadi kubwa ya wateja ikiwemo wakinamama wanaofika kujifungua.
Ujenzi wa wodi hii ya wazazi ulianza mwezi wa sita mwaka 2022 ambapo hadi sasa kimetolewa kiasi cha Tsh Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo ambapo kiasi cha Tsh Milioni 50 kilitolewa kwa awamu ya kwanza na kufikisha ujenzi katika hatua ya lenta, na awamu ya pili imetolewa kiasi cha Tsh Milioni 50 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo kwa hatua zinazofuata.
Wodi hii itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kulaza wakina mama 30 waliojifungua kwa wakati mmoja na hivyo kusaidia kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wakinamama wanaokuja kupata huduma hiyo katika kituo hiki.
Takribani wakina mama 610 hujifungua kwa mwezi katika kituo hiki cha afya cha Buzuruga.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.