" Kukamilika kwa miradi hii ya afya sio kwa ajili ya watu flani,ni kwa manufaa ya wote.Watakaotibiwa hapa ni watanzania wote, maendeleo hayana chama wote tuwe kitu kimoja kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati. "
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Ilemela Mhe.Angelina Mabula ambaye pia ni Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo alipotembelea zahanati ya Nyakato, Nyambiti, Kawekamo na Luhanga kuona ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea ambako kote mfuko wa jimbo umechangia katika utekelezaji wake.
Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 83.7 ya mfuko wa jimbo imetumika kwa mwaka wa fedha 2022/2023 katika miradi mbalimbali ya maendeleo Ilemela.
Mhe.Mabula amesisitiza kazi kufanyika kwa ushirikiano kwa ngazi zote kupitia nguvu ya utatu kwa maana ya wananchi,serikali/wataalam na viongozi na Mbunge/Chama kwani ni muhimu kuunganisha nguvu katika kufanikisha mipango ya kuleta maendeleo Ilemela.
Nae Mstahiki Meya Mhe.Renatus Mulunga ameuhakikishia umma kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ipo tayari kuunga mkono kukamilisha ujenzi wa maboma ya miradi mbalimbali yaliyoanzishwa na wananchi kwa wakati ili huduma zilizokusudiwa zianze kutolewa mara moja.
Sambamba na hilo mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwaloni yenye urefu mita 900 umetembelewa huku Mhe.akipongeza kazi nzuri ya kurahisisha mawasliano kupitia miundo mbinu ya barabara inayoendelea jimboni mwake.
Aidha Mhe.Mabula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya I wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea nayo kwa kutoa fedha nyingi kuanzisha na kukamilisha miradi ya maendeleo huku akiwasihi wananchi kuunga mkono juhudi hizo zenye manufaa makubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Ismail Bundala ni mkazi wa kata ya Kiseke mahali zahanati ya Luhanga ilipo yeye anapongeza maboresho ya huduma za afya yanayoendelea katika zahanati hiyo.
" Mke wangu mwaka jana aliponea hapa , alipata changamoto ya ujauzito kutaka kuharibika tukiwa nyumbani usiku tulikimbilia hapa na kupata matibabu na mwezi uliopita tumepokea mtoto wetu wa tatu hapa hapa zahanati ya Luhanga.Mama anaupiga mwingi kwa kweli."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.