Jumla ya vijana 75 wakike wakiwa 12 na wakiume 63 wamehitimu mafunzo ya uaskari wa jeshi la akiba maarufu mgambo ndani ya wilaya ya Ilemela.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoanza mapema Agosti 05, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Salum Kali amewataka vijana hao kuendelea kuwa waadirifu na wazalendo kwa nchi yao pamoja na kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa maslahi ya taifa ikiwemo kuendelea kudumisha ulinzi na usalama wanchi na raia wake.
‘.. Nendeni mkawe walinzi wa usalama wa nchi yetu na raia wake, Kabla mtu hayaleta chokochoko zozote nyie muwe teyari mshapata taarifa na kuchukua hatua ..’ Alisema
Aidha Mhe Kali ameyataka makampuni ya ulinzi, vyombo vyengine vya usalama na taasisi za Serikali hasa manispaa ya Ilemela kuwatumia vijana hao kwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo kusimamia usalama na ulinzi wa mitihani, kusimamia ulinzi wa matukio mbalimbali ya shughuli za Umma ili kutoa fursa kwa vijana hao kujipatia ajira na kipato.
Kwa upande wake mshauri wa jeshi la akiba wilaya ya Ilemela Kanali Evans Akili amefafanua kuwa madhumuni ya mafunzo ya jeshi la akiba ni kusogeza huduma za ulinzi karibu na wananchi, kushirikisha wananchi katika suala zima la ulinzi wa taifa, kumuandaa askari wa jeshi la akiba kuingia vitani wakati wowote wa vita pindi nchi itakapovamiwa pamoja na kujifunza mbinu za kivita na mikakati ya kukabiliana na adui.
Nice Jacob Binyaruka ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba akitokea kata ya Ilemela, ambapo amepongeza na kushukuru kwa kupata mafunzo huku akiiasa jamii kuondoa fikra potofu kwa jinsia ya kike kushindwa kushiriki mafunzo ya kijeshi sanjari na kuomba jamii kuendelea kuwaruhusu vijana wao kujitokeza kupata mafunzo kwaajili ya kulinda taifa na uzalendo
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri Ya Manispaa ya Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.