Ni takwa la serikali kurahisisha mchakato wa manunuzi ngazi zote za vituo vya umma ambako huduma zinatolewa na kuhakikisha kuwa kila taarifa ya manunuzi na utendaji wake vinakuwa kwenye maandishi na kutunzwa kwa marejeo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo cha manunuzi na ugavi cha Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Nestory Mkama wakati wa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa ununuzi kwa taasisi za umma (NeST) kwa walimu wakuu wa shule za msingi na watendaji wa kata wa Manispaa ya Ilemela.
Akifafanua sheria ya manunuzi ya mwaka 2023 sambamba na kanuni zake za mwaka 2024 ambayo inatoa misingi inayoongoza manunuzi ya vifaa mbalimbali na matumizi ya rasilimali za ndani "force account" katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi huku akibainisha kuwepo kwa adhabu endapo kutakuwa na ukiukwaji wa sheria hiyo.
"...faini ,kifungo au kufilisiwa mali kufidia hasara iliyosababishwa ni miongoni mwa adhabu zilizotajwa.Tuepukane na hayo kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake."Amesema Mkama
Kaimu Mkuu wa kitengo cha TEHAMA cha Halmashauri hiyo Mussa Zuberi ameahidi ushirikiano mkubwa kwao kutoka timu nzima ya kitengo cha TEHAMA kwa lengo la kufanikisha mchakato mzima kuanzia usajili wao katika mfumo huo wa NeST ulioboreshwa kwa ngazi zao kulingana na mahitaji ya maeneo husika.
Mwl.Vedastus Deogratius ni mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Songambele iliyopo kata ya Kirumba amekiri kuwa mfumo huo ni mzuri na umekuja kurahisisha shughuli za manunuzi kwani kila kitu kitakuwa kwenye maandishi na kitaingia kwenye mfumo.
"Naamini miradi yetu sasa itakamilika kwa wakati."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.