" Ni mpango wa serikali kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za kifedha ikiwemo matumizi yake yanafanyika kidijitali kupitia mifumo mbalimbali ya TEHAMA kwa uwazi mkubwa pamoja na upatikanaji wa taarifa wakati wowote ikiwa ni moja ya njia ya kupunguza mianya ya upotevu wa fedha na kuongeza kasi ya uwajibikaji na kupata matokeo chanya kwa wakati."
Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Ilemela Isack Tanguye wakati akitoa mafunzo ya mfumo wa "FFARS" kwa watendaji wa kata zote 19 zinazounda Manispaa ya Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia kitengo cha TEHAMA imetoa mafunzo juu ya mfumo wa FFARS ambao unaendelea kutumika katika vituo vya kutolea huduma mbalimbali za kijamii.
" Facility Financial Accounting and Reporting System "FFARS" ni mfumo wa kihasibu wa kifedha na utoaji taarifa maeneo ya vituoni ambako shughuli/huduma mbalimbali za fedha zinatolewa mfano shuleni na vituo vya kutolea huduma za afya. " Amesema Tanguye.
Nae mhasibu wa mfumo wa FFARS Manispaa ya Ilemela Bi.Philimina Tibaijuka amebainisha faida za mfumo huo ni upatikanaji wa taarifa kwa wakati sambamba na uwazi wa kila kinachofanyika kifedha katika eneo mfumo unapotumika.
Bernadetha Charles ni mtendaji wa kata ya Ibungilo yeye anashukuru uongozi kwa mafunzo hayo yenye manufaa makubwa katika utendaji wao wa kazi.
"Naishukuru serikali na uongozi wa Manispaa kwa kutupatia mafunzo haya kwani yatatusaidia sana kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye kata na pia itatupunguzia hoja za kiukaguzi kwani mfumo utaonyesha namna pesa ilivyotumika."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia kitengo cha TEHAMA imetoa mafunzo juu ya mfumo wa FFARS ambao unaendelea kutumika katika vituo vya kutolea huduma mbalimbali za kijamii.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.