WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUTUNZA MALI ZA UMMA
Watendaji wa kata wametakiwa kuwa makini na waadilifu katika kutunza mali mbalimbali za umma wanazokabidhiwa .Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela , Ndugu John Wanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya pikipiki Saba kwa watendaji wa kata za Nyasaka, Nyamhongolo, Sangabuye, Shibula, Kahama, Bugogwa na Kayenze yaliyofanywa na Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya Mwenyekiti wake na Mstahiki Meya wa Manispaa Ilemela Mheshimiwa Renatus Mulunga
“Tumewakabidhi pikipiki hizi ili kurahisisha utendaji kazi wa shughuli zenu na kuongeza ufanisi, Ila nawaomba mkatunze mali hizi za umma nadhani mmeona kwenye ile karatasi mmesaini maana yake ikipotea au ukiharibu kwa makusudi utawajibika, Sisi hatutamvumilia mtu yeyote atakayeigawa pikipiki kwa mtu asiyehusika hizi ni pikipiki za kisasa zinapendwa na wengi muwe makini zisiibiwe”
Akizungumza kwa niaba ya watendaji walionufaika na pikipiki hizo mtendaji wa kata ya Nyamhongolo Victor Leonard mbali na kuishukuru Manispaa kwa kuona changamoto waliokuwa wanaipata katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, na kuamua kuitatua ameahidi kuwa makini na muadilifu katika kutunza pikipiki aliyokabidhiwa na kuongeza kuwa makabidhiano hayo ya pikipiki yataenda kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.
Pikipiki hizo zilizogharimu jumla ya kiasi ya fedha za Kitanzania Tsh. 17,010,000 zimenunuliwa kupitia fedha iliyotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.