• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Maadili ya Msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utumishi na Utawala
        • Mipango na ufuatiliaji
        • Kilimo, Ufugaji na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Sekondari
        • Elimu ya Awali na Msingi
        • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
        • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Miundombinu na Uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Vitengo
        • Mazingira na Usafishaji
        • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
        • Michezo, Utamaduni na Sanaa
        • Fedha na Uhasibu
        • Sheria
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Manunuzi
        • TEHAMA na Takwimu
        • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA WATOTO WANACHANJWA

Posted on: December 2nd, 2022

Wazazi na walezi Wilayani Ilemela wametakiwa kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri kuanzia mwezi 0 hadi miezi 59 wanapatia chanjo ya polio ili kuwakinga na ugonjwa huu ambao hauna tiba kwani chanjo hii ni salama kabisa.


Wito huo umetolewa na Ndugu Said Kitinga (Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela) akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilemela wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio awamu ya nne ambayo ilifanyika katika kituo cha afya Buzuruga


“Chanjo hii ni salama, hivyo niwaase wazazi na walezi kuhakikisha  watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano (mwezi 0 hadi miezi 59) wanapatiwa  chanjo na pasiwepo na mtoto wa kuachwa kupelekwa kwenye chanjo ili kuweza kuwakinga watoto wetu kwani nao wana haki ya kuishi”, alisema Ndugu Kitinga


Aidha aliendelea kutoa wito wa kuupiga vita ugonjwa huu wa polio, kwani ni ugonjwa mbaya kwasababu hauna matibabu na dawa yake ni chanjo hivyo mtoto mdogo asipochanjwa unamuweka katika hali hatarishi ya kupata ugonjwa huu ambao hupelekea kupooza au kifo.


“Serikali inaendelea kutenga fedha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya duniani na Shirika la UNICEF katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora kuanzia wakiwa watoto wadogo”, alisema Ndugu Kitinga


Sambamba na hayo amewapongeza wakinamama waliojitokeza kwani itakuwa chachu kwa wakinamama wengine ili waweze kujitokeza katika zoezi la chanjo  huku akitoa tahadhari kwa watu wanaohusisha mazoezi ya chanjo na taarifa ambazo sio rasmi, wanatumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa potofu matokeo yake huleta taharuki katika mazoezi ya kitaifa na kuwataka  iwapo itatokea mtu mwenye nia ovu taarifa itolewe kwa viongozi


Prisca James mwenye watoto wanne akitokea kata ya Mecco ni mmoja wa wazazi waliofika katika kituo cha Afya  kwa ajili ya kumleta mtoto wake ili apatiwe chanjo ya Polio kwani ameelimishwa umuhimu wake hivyo amewataka wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani chanjo ni salama na haina madhara yoyote


Damaris Dawson mratibu wa chanjo kituo cha afya Buzuruga, ametoa wito kwa wakina mama kujitokeza kwani chanjo ni salama huku akiomba ushirikiano kwa wazazi na walezi watakaokuwa nyumbani kwani wataalam wa afya wanapita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo.





Announcements

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2022 SHULE ZA SERIKALI NA BINAFSI MANISPAA YA ILEMELA January 29, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA September 30, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA JULAI-SEPTEMBA 2022 October 11, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022 December 01, 2022
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • ILEMELA YAKIDHI VIGEZO VYA KUTEKELEZA MIRADI MINNE

    January 19, 2023
  • ELIMU YA MATUMIZI BORA YA FEDHA YATOLEWA KWA WANUFAIKA WA MKOPO WA ASILIMIA 10

    January 18, 2023
  • DC ILEMELA APIGA MARUFUKU MICHANGO KIDATO CHA KWANZA

    January 17, 2023
  • MKUU WA MKOA WA MWANZA AIPONGEZA ILEMELA UKAMILISHAJI WA VYUMBA VYA MADARASA

    December 22, 2022
  • Tazama zaidi

Video

SHULE YA SEKONDARI BUZURUGA ILIYOJENGWA KWA FEDHA ZA SEQUIP
More Videos

Quick Links

  • Kuhakiki Taarifa za Mpiga Kura
  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip
  • Maombi ya leseni ya biashara

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.